Общество с ограниченной ответственностью Издательско-торговая корпорация "Дашков и К". 2018. 411 с.
Afrika, bara lenye utajiri wa tamaduni anuwai na maliasili, linakabiliwa na changamoto nyingi kijamii, kiuchumi na kisiasa. Umaskini, njaa, maradhi, migogoro ya kisiasa, kiwango cha juu cha vifo na makadirio ya chini ya umri wa kuishi,hizi siyo changamoto zinazoikumba Afrika, bali ni matatizo yanayotokana na changamoto halisi, zinazoikumba Afrika. Makala hii inalenga kuhamasisha vijana na Waafrika kwa ujumla, katika kutekeleza Ajenda ya Afrika mpya kuelekea 2063. Aidha,inachunguza changamoto na matarajio ya Afrika ya sasa, na kutoa mapendekezo yenye mlengo wa kujenga Afrika yenye nguvu, mshikamano na maendeleo endelevu.[2]